1. Utangulizi & Makubaliano
Karibu kwenye Kilimo Ardhi β Jukwaa la Ushauri wa Kilimo linalotumia teknolojia ya kisasa ya sensor za kupima udongo kusaidia wakulima wa Tanzania kupata mapendekezo ya mbolea yanayoendana na ardhi zao kutokana na mazao yake.
Masharti haya ya huduma ("Masharti") yanafunga mkataba kati yako ("Mtumiaji") na Kilimo Ardhi ("Kampuni", "Sisi"). Kwa kutumia jukwaa letu kwa njia yoyote programu ya simu au SMS unakubali kufuata masharti haya yote.
β οΈ Muhimu Sana: Tafadhali soma masharti haya kwa makini kabla ya kuanza kutumia huduma. Kama hukubaliani na masharti yoyote, tafadhali usitumie huduma zetu.
β
Inazingatia Sheria ya Tanzania
β
Inatumika kwa Wakulima Wote
π Makubaliano ya Kisheria
2. Masharti ya Kujiunga
2.1 Unastahili Kutumia Huduma Kama:
- Una umri wa miaka 18 au zaidi
- Una uwezo wa kisheria wa kufwata mikataba nchini Tanzania
- Unatoa taarifa sahihi na za kweli wakati wa kujiandikisha
- Hujawahi kusimamishwa kutoka kwa huduma zetu hapo awali
2.2 Kwa Watumiaji Wadogo
Kama una umri kati ya miaka 13 na 17, unaweza kutumia huduma hii tu kwa idhini ya mzazi au mlezi wako wa kisheria. Mzazi au mlezi anapaswa kukubali masharti haya kwa niaba yako.
π« Marufuku: Huduma hii hairuhusiwi kwa watoto walio chini ya miaka 13. Kama itabainika kuwa mtumiaji ana umri chini ya huo, akaunti itafutwa mara moja.
3. Huduma Tunazotoa
3.1 Huduma Kuu
- Mapendekezo ya Mbolea: Ushauri wa kisayansi wa aina na kiasi cha mbolea kulingana na aina ya zao na udongo wako baada ya kufanya vipimo
- Vipimo vya Udongo: Uchambuzi wa matokeo ya vipimo vya udongo na ushauri unaotokana navyo kwa kulima bora
- Nunua Mbolea: Nunua mbolea moja kwa moja kwa wauzaji waliodhibitishwa kisheria na wamejisajili kwa Kilimo Bando - mfumo unaoimilikiwa na Bizy Tech Limited. Huduma hii inawalipwa na wakulima na wauzaji wa kilimo (agro dealers)
- Nunua Mbegu: Nunua mbegu bora moja kwa moja kutoka kwa wauzaji waliodhibitishwa kisheria na wamejisajili kwa Kilimo Bando - mfumo unaoimilikiwa na Bizy Tech Limited. Huduma hii inawalipwa na wakulima na wauzaji wa kilimo (agro dealers)
- Upimaji wa Ukubwa wa Shamba: Upimaji wa GPS kwa ajili ya kujua ukubwa halisi wa shamba lako na kupanga matumizi ya ardhi
3.2 Mipaka ya Huduma
Huduma zetu zinategemea teknolojia na data zinazopatikana. Tunajitahidi kutoa huduma bora, lakini hatuwezi kuhakikisha kwamba:
- Huduma itakuwa inapatikana wakati wote bila kukatizwa
- Matokeo ya mapendekezo yatathibitishwa na mtaalamu wa kilimo kwa kila kesi
- Bei za mbolea au mbegu hazitabadilika
πΎ Kumbuka: Mapendekezo yetu yanasaidia kufanya maamuzi bora, lakini hayabadilishi ushauri wa mtaalamu wa kilimo aliyeidhinishwa. Mkulima ana jukumu la mwisho la maamuzi ya shamba lake.
4. Akaunti na Uwajibikaji
4.1 Uundaji wa Akaunti
Kujiandikisha, unahitaji kutoa:
- Jina kamili lako halisi
- Nambari ya simu inayofanya kazi
- Eneo (Mkoa, Wilaya, Kata au Kijiji)
- Barua pepe (si lazima lakini inashauriwa)
4.1a Wakulima Waliosajiliwa Tayari
Kama wewe ni mkulima uliefanyia uliyesajiliwa serikalini na una Nambari ya Usajili wa Mkulima, unaweza kuingia moja kwa moja bila kujiandikisha tena. Tumia:
- Nambari yako ya Usajili wa Mkulima (Farmer Registration Number)
- Nenosiri: Nambari yako ya simu iliyosajiliwa hapo awali
Hii ni njia haraka kwa wakulima waliosajiliwa tayari. Huwezi kuunda akaunti mpya kwa kutumia nambari yako ya usajili ni kwa kuingia tu.
π Nambari ya Usajili wa Mkulima: Inapatikana kwenye chipukizi chako au kumkumbusha kwa huduma. Kama umechelewa kupata yako, wasiliana nasi.
4.2 Usalama wa Akaunti Yako
Wewe ndiye unayewajibika kwa usalama wa akaunti yako. Masharti haya yanakusaidia kuelewa wajibu huu:
- Usishirikishe nenosiri lako na mtu yeyote
- Tujulishe mara moja kama unashuku kuwa mtu mwingine ameingia akaunti yako: +255 XXX XXX XXX
- Unatakiwa kutoka nje ya akaunti yako kila unapotumia simu au kompyuta ya pamoja
- Kila shughuli inayofanywa kupitia akaunti yako inabeba jukumu lako isipokuwa uthibitishwe vinginevyo
οΏ½ Akaunti Nyingi Zinakubalika: Unaweza kuwa na akaunti nyingi kwa ajili ya mafarms tofauti au mahitaji tofauti. Kila akaunti lazima itoe taarifa sahihi na inaweza kumaanisha muamala tofauti wa malipo kwa kila akaunti.
5. Malipo na Michango
5.1 Bei na Ada
Kilimo Ardhi hutoa mchanganyiko wa huduma za bure na za kulipwa. Mapendekezo ya kina ya mbolea yanayoandaliwa maalum kwa shamba lako yanalipwa.
| Huduma |
Aina |
Maelezo |
| Usajili wa akaunti |
π Bure |
Kuunda akaunti na kuangalia taarifa za jumla |
| Mapendekezo ya mbolea |
π³ Inalipiwa |
Uchambuzi kamili na mapendekezo maalum kwa shamba lako |
| Uchambuzi wa udongo |
π³ Inalipiwa |
Matokeo ya vipimo na ushauri maalum |
| Nunua Mbolea |
π³ Unalipia kwa Agro dealer |
Nunua mbolea kwa wauzaji kupitia Kilimo ardhi ikiwa tumeunganisha na Kilimo Bando (Bizy Tech Limited). Walipwa na wakulima na wauzaji wa kilimo |
| Nunua Mbegu |
π³ Unalipia kwa Agro dealer |
Nunua mbegu kwa wauzaji kupitia Kilimo Bando (Bizy Tech Limited). Walipwa na wakulima na wauzaji wa kilimo |
| Upimaji wa Ukubwa wa Shamba |
π³ Inalipiwa |
Upimaji wa GPS na ripoti ya ardhi |
5.2 Njia za Malipo Zinazokubaliwa
π± M-Pesa
π± Airtel Money
π± HaloPesa
π± Mixx by Yas
π΅ Pesa Taslimu
Kumbuka: Huduma za "Nunua Mbolea" na "Nunua Mbegu" zinafanywa chini ya mfumo wa Kilimo Bando unaoimilikiwa na Bizy Tech Limited. Huduma hizi zinaweza kuwalipwa na wakulima, wauzaji wa kilimo (agro dealers), au hao wote. Malipo kwa mbolea na mbegu maalum yatakuwa kati yako, mzauji, au kwa mujibu wa mupatanishi wa mfumo wa Kilimo Bando. Kilimo Ardhi inatoa huduma ya kuunganisha na kuandaa platform kwa huduma hii.
5.3 Sera ya Kurejesha Pesa
- Kama huduma haikutolewa: Pesa itarudishwa kikamilifu ndani ya saa 48
- Tatizo la kiufundi kutoka kwetu: Pesa itarudishwa au huduma itatolewa tena bila malipo
- Kama mkulima alitoa taarifa potofu: Pesa haitarudishwa kwa sababu mapendekezo yaliweza kutolewa kwa taarifa zilizotolewa
- Ombi la kurudisha pesa: Lazima liwasilishwe ndani ya siku 7 baada ya malipo
β οΈ Bei zinaweza kubadilika: Tutakujulisha mapema kupitia SMS au barua pepe kabla ya mabadiliko yoyote ya bei.
6. Mapendekezo ya Mbolea β Masharti Maalum
6.1 Msingi wa Mapendekezo Yetu
Mapendekezo yanayotolewa na Kilimo Ardhi yanazingatia:
- Taarifa unazozitoa wewe mwenyewe (aina ya zao, ukubwa wa shamba)
- Matokeo ya vipimo vya udongo (kama yalitolewa)
- Mwongozo wa kisayansi wa kilimo uliothibitishwa
6.2 Mipaka ya Mapendekezo
Mapendekezo ya Kilimo Ardhi ni mwongozo wa kusaidia maamuzi si amri za lazima kufuatwa. Kampuni haiwajibiki kwa:
- Hasara ya mazao inayotokana na hali za nje kama ukame, mafuriko, au wadudu
- Matokeo yasiyotarajiwa yatokanayo na taarifa potofu ulizotupa
- Mabadiliko ya bei ya mbolea baada ya mapendekezo kutolewa
- Kutofuata mapendekezo kwa usahihi
πΏ Ushauri wa Pamoja: Tunapendekeza daima kushauriana na afisa wa kilimo wa kata au wilaya yako kwa maamuzi makubwa ya shamba, hasa kwa ardhi kubwa au mazao ya biashara.
7. Matumizi Yanayoruhusiwa
7.1 Unatakiwa UFANYE:
- β
Tumia huduma kwa madhumuni ya halali ya kilimo
- β
Toa taarifa sahihi na za kweli kuhusu shamba lako
- β
Lipa ada zinazohusika kwa wakati
- β
Ripoti matatizo yoyote ya kiufundi kwa timu yetu
- β
Usishirikishe nenosiri au taarifa za akaunti yako na mtu mwingine
7.2 MARUFUKU KABISA β Usifanye:
- π« Kutoa taarifa za uongo au za kupotosha kwa makusudi
- π« Kutumia huduma kwa njia yoyote ya udanganyifu au kupiga watu wengine
- π« Kujaribu kuingia kwenye mifumo yetu kwa njia zisizoidhinishwa (hacking)
- π« Kushirikiana na watu wengine kuingia kwenye akaunti zako au kutumia nenosiri lako
- π« Kuuza au kushiriki mapendekezo yako na watu wengine kwa faida ya kibiashara bila idhini yetu
- π« Kutumia zana za kiotometi (bots) kuchimba data kutoka kwenye mfumo wetu
- π« Kueneza habari za uongo kuhusu mbolea au kilimo kwa kutumia jina letu
π¨ Matokeo ya Ukiukaji: Ukiuka masharti haya, akaunti yako inaweza kusimamishwa mara moja, na tunaweza kuchukua hatua za kisheria endapo uharibifu mkubwa ulisababishwa.
8. Umiliki
8.1 Kinachomilikiwa na Kilimo Ardhi
Kilimo Ardhi inamiliki kikamilifu:
- Msimbo wa programu (source code) wa mfumo wetu wote
- Muundo wa mfumo (UI/UX design) ya tovuti na programu ya simu
- Algorithms na mifano ya akili bandia tunayotumia kutoa mapendekezo kwa ushirikiano na Kilimo Bando
- Jina, nembo (logo) na alama za biashara (trademark) za Kilimo Ardhi
- Maudhui yote ya elimu ya kilimo yaliyoundwa na timu yetu
8.2 Kinachomilikiwa na Wewe (Mtumiaji)
- Taarifa zako za kibinafsi unazotupa
- Picha na nyaraka unazopakia kwenye mfumo
- Historia ya shamba lako na mazao yako
8.3 Ruhusa Unayotupatia
Kwa kutumia huduma zetu, unatupa ruhusa ya kutumia data yako (bila jina lako) kwa:
- Kuboresha algorithms na mifano yetu ya mapendekezo
- Kutengeneza ripoti za jumla za kilimo nchini Tanzania (bila kutaja jina lako)
- Utafiti wa kisayansi wa kilimo unaofanywa na washirika wetu waliothibitishwa
π Faragha Kwanza: Taarifa zako hazitashirkishwa na jina lako. Ripoti zote zinatumia takwimu za jumla (aggregate data) tu. Angalia
Sera yetu ya Faragha kwa maelezo zaidi.
9. Mipaka ya Uwajibikaji
9.1 Tunawajibika Kwa:
- β
Kutoa mapendekezo kwa uaminifu kulingana na taarifa ulizotupa
- β
Kulinda taarifa zako kwa mujibu wa Sera yetu ya Faragha
- β
Kujibu malalamiko na matatizo ndani ya muda uliowekwa
- β
Kurejesha pesa pale ambapo huduma haikutolewa
9.2 Hatuwajibiki Kwa:
- πΈ Hasara ya mazao inayotokana na hali za asili (mvua kubwa, ukame, baridi kali)
- πΈ Maamuzi ya mwisho ya mkulima ambayo yalitofautiana na mapendekezo tuliyotoa
- πΈ Tatizo linalotokana na mitandao ya simu au huduma za malipo za wahusika wengine
- πΈ Hasara inayotokana na kutumia taarifa za kampuni nyingine zilizoshirikishwa
- πΈ Kupoteza mapato au faida kwa njia yoyote inayohusiana na matumizi ya huduma zetu
βοΈ Kiwango cha Fidia: Kama tutawajibika kwa sababu yoyote, kiasi cha fidia hakitazidi jumla ya malipo uliyolipa katika miezi 3 iliyopita.
10. Kusimamisha Huduma
10.1 Unaweza Kusimamisha Akaunti Yako Wakati Wowote
Piga simu, tuma ujumbe au wasiliana nasi kupitia barua pepe kuomba akaunti yako ifutwe. Tutafanya hivyo ndani ya siku 5 za kazi.
10.2 Tunaweza Kusimamisha Akaunti Yako Kama:
- Umekiuka masharti haya
- Umetoa taarifa za uongo kwa makusudi
- Akaunti yako imetumika kwa shughuli za udanganyifu
- Haujalipia huduma baada ya kukumbushwa mara tatu
- Mifumo ya kisheria imehitaji kufanya hivyo
10.3 Baada ya Kusimamishwa
- Data yako itahifadhiwa kwa miezi 6 (kwa malengo ya kisheria)
- Unaweza kuomba nakala ya data yako ndani ya muda huo
- Malipo yaliyofanywa kabla ya kusimamishwa hayatarudishwa isipokuwa kukiwa na tatizo kutoka kwetu
- Baada ya miezi 6, taarifa zako zitasimbwa fiche kabisa
11. Utatuzi wa Migogoro
11.1 Hatua za Kwanza
Kabla ya kuchukua hatua yoyote ya kisheria, tunakuhimiza kufuata njia hizi kwa mpangilio:
- Wasiliana Nasi Moja kwa Moja: Piga simu au tuma barua pepe tutajaribu kutatua tatizo ndani ya saa 72
- Kuomba Usuluhishi: Kama hatujatatua tatizo, tunaweza kupendekeza msuluhishi wa tatu asiye na upande
- Uamuzi wa Kisheria: Kama yote yameshindwa, migogoro itasimamiwa na mahakama za Tanzania
11.2 Sheria Inayotumika
Masharti haya yanafuata sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiwemo:
- Sheria ya Mikataba ya Tanzania
- Sheria ya Kulinda Watumiaji (Consumer Protection Act)
- Sheria ya Mawasiliano ya Elektroniki Tanzania
- Kanuni za TCRA zinazohusiana na huduma za kidijitali
π€ Tutajaribu Maridhiano: Tunaamini migogoro mingi inaweza kutatuliwa kwa mazungumzo ya amani. Wasiliana nasi kwanza β tunajali wateja wetu na tutajaribu kutafuta suluhisho la haki kwa pande zote.
12. Mabadiliko ya Masharti
Kilimo Ardhi inaweza kubadilisha masharti haya mara kwa mara ili kuonyesha:
- Huduma mpya tunazozindua
- Mabadiliko ya sheria na kanuni za Tanzania
- Uboreshaji wa sera za kampuni
- Maoni ya wateja wetu
12.1 Jinsi Utakavyojulishwa
- π± Ujumbe wa SMS kwa nambari yako iliyosajiliwa
- π§ Barua pepe (kama uliitoa)
- π Arifa ndani ya programu (in-app notification)
- π Tangazo kwenye wavuti yetu
12.2 Kukubali Mabadiliko
Utajulishwa angalau siku 14 kabla ya mabadiliko makubwa kuanza kutumika. Kuendelea kutumia huduma baada ya tarehe hiyo kunamaanisha umekubali masharti mapya. Kama hukubaliani, una haki ya kusimamisha akaunti yako bila malipo yoyote ya ziada.
π Daima Angalia: Toleo la sasa la masharti litakuwepo daima kwenye wavuti yetu. Tarehe ya kusasishwa itaonekana juu ya ukurasa huu.